Kocha mkuu wa Manchester United aeleza ya moyoni kuhusiana na mfululizo mbaya wa matokeo ya klabu ya Manchester United katika kipindi hiki.
Akiongea na waandishi wa habari alisema ya kuwa mfululizo huo wa matokeo mabovu katika mechi 6 zilizopita umewafanya mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na imani na Kocha huyo na hivyo kuwafanya wengi kumzungumzia yeye juu ya hali hiyo ila yeye anachokijali ni sapoti ya wachezaji tu na hivyo haimkatishi tamaa kusonga mbele kama jinsi inavyotabiliwa.
Katika siku ya jana mmiliki wa PSG amekana habari hizo na kusema hawajaweka mazungumzo yeyote na Relal Madrid juu ya kumsajili mchezaji huyo ambaye kwa sasa amekuwa katika kiwango cha chini sana tofauti na alivyokuwa katika misimu iliyopita
Kocha mkuu wa Manchester City Pellegrini amekuwa katika wasiswasi mkubwa mara baada ya Manchester City kujaribu kuweka mazungumzo na kocha wa Buyern Munichen kuifundisha timu hiyo.
Katika maelezo yake kocha huyo muda sio mrefu akiongea na waandishi wa habari asema ya kuwa ana Guardiola ndiye kocha atakayeifundisha timu hiyo muda sio mrefu katika kipindi kijacho huku akimtakia mema katika kazi yake ya ukocha na pili akitambua ya kuwa kocha huyo ni moja ya makocha wenye uwezo mkubwa katika ulimwengu wa kandanda
Kumekuwa na tetesi nyingi katika magazeti mengi duniani ya michezo kuhusu Mourinho ambapo mengi yalielezea ya kuwa huenda kocha huyo atapumzika kidogo katika soka ili kuweza kujipanga upya katika fani yake kitu ambacho sicho. Leo hii Mourinho amedhihirisha ya kuwa anapenda kuendelea na Soka na hivyo hatachukua mapumziko huku akionekana kupenda kuendelea kufundisha Uingereza na sio nje ya hapo kama jinsi ilivyoelezwa na baadhi ya magazeti.
Aliekuwa kocha wa zamani wa Chelesea Guus hiddink aonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kuchukukua jukumu la kuifundisha Klabu ya Chelsea.
Katika maelezo yake kocha huyo pindi akihojiwa na moja ya jarida la michezo alisema kuwa hali ya Chelsea kwa sasa ni mbaya sana na hana uhakika ya kuwa ataweza kuifundisha timu hiyo lakini anaamini ataifundisha timu hiyo endapo ataijua sababu ya kusababisha timu hiyo kushuka kiwango msimu huu.
Guus Hiddink amekuwa habari kubwa katika mitandao mingi ya kijamii na ile ya soka kwa kupewa nafasi kubwa ya kuweza kuifundisha Chelsea kutokana na mafanikio ambayo aliwahi kuyafanya katika timu hiyo
Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amshukuru sir Alex Ferguson juu ya ushauri alioutoa kwa mmiliki wa Chelsea zidi yake.
Katika siku zilizopita Ferguson alimsisitiza mmiliki wa Chelsea kutomfukuza Mourinho kwa kuwa ni kocha mwenye kipaji katika ulimwengu wa Soka huku akimsisitiza kutotofanya hivyo akiamini ya kuwa hiki ni kipindi kifupi tu kinachoikumba timu hiyo na kuwa njia ya kufukuza kocha sio tiba juu ya hali hiyo kwa kuwa ni makocha wengi waliofukuzwa humo na haijamaliza tatizo la kimpira katika klabu hiyo, Ferguson alisisitiza ya kuwa ni kumpa fursa kocha huyo ili aweze kutengeneza timu hiyo.
Kwa maneno hayo yalimpa nguvu Mourinho na hivyo kuamini ya kuwa Ferg ndiye rafiki wa kweli kwake maana amemfariji yeye na mashabiki wote katika klabu hiyo katika kipindi hiki cha mpito.
Mshambuliaji wa timu ya Real Madrid Christian Ronaldo avunja tena rekodi katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Katika rekodi hii Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha magori 10 katika mzunguko wa makundi katika ligi ya mabingwa Ulaya, rekodi imevunja katika mechi ya jana ya mzunguko wa ligi hiyo mara baada ya kupachika magori 4 ambapo katika mechi hiyo Real Madrid ilishinda magori 8 zidi ya Malmo
Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na ile ya Real Madrid Ancelotti afunguka kuhusu nia yake ya kupenda kuifundisha Manchester United katika kipindi hiki.
Alipohojiwa na mmoja wa wahandishi wa habari za michezo alisema ya kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati ya kuifundisha Manchester United toka muda mrefu na hivyo itakuwa ni vizuri kwake endapo atachaguliwa kwenda kuifundisha timu hiyo katika kipindi hiki kwa kuwa bado anapenda kufundisha soka nchini Uingereza.
Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid Griezmann afunguka kuhusu uamuzi wake mara baada ya kuwekwa katika moja ya usajili ambao Chelsea imepanga kuufanya mwezi wa kwanza.
Akiongea na moja ya jarida la michezo nchini Uhispania ameeleza ya kuwa ana furaha kuichezea timu hiyo na haoni sababu ya kuiama huku akisistiza ya kuwa anajisikia furaha kuichezea klabu yake hiyo ya Atletico Madrid na hivyo hatokubali kusajiliwa katika kipindi hiki