EDEN HAZARD; Mourinho amenihimarisha!
Kiungo mshambuliaji wa timu ya chelsea na timu ya ubeligiji amemsifia kocha wake wa timu ya klabu Jose Mourinho kwa kuihimarisha chelsea kimtazamo na yeye mwenyewe,
Msimu uliopita chelsea iliweza kuwa chini ya kocha huyo mreno na kuhimarishwa vyema katika ligi hiyo uingereza, japokuwa katikati kulikuwa na kutokuelewana kimtazamo wa mafunzo ya mchezo kati ya kocha huyo na hazard lakini tofauti ziliisha tu mara baaada ya kufikia katika hali ya mafanikio ambapo katika msimu huu chelsea imeweza kuongoza ligi katika kipindi kirefu,
Mbali na hayo Eden Hazard alisema haya;
``Ni kweli kuna mahusiano mazuri baina yetu, kitu kizuri kwake ni kimoja, anaruhusu mchezaji kutumia uwezo wake mwenyewe, hawi upande wangu muda wote, ninakubaliana na yeye kwa kuwa muda wote yeye anaelekeza tu kitu cha kufanya,
Mbali na hayo Chelsea imeweza kuwa na unafuu katika timu za uingereza katika michuano ya mabingwa ulaya UEFA, na wiki ya karibun itakipiga na timu ya PSG katika uwanja wake wa nyumbani.