Yanga yazidi kugawa kipigo
Timu ya yanga leo imeweza kuifunga mbeya city magori matatu kwa moja( 3-1). Timu hiyo ya jangwani iliweza kuifunga Mbeya city magaro matatu ambapo bao moja liliweza kupatikana dakika ya 18 na simon msuva akimalizia pasi nzuri kwa kichwa kutokea kwa niyonzima.
Pia katika kipindi cha pili dakika ya 59 Mrisho Ngassa aliweza kuifungia timu yake bao la pili na kuifanya iweze kuwadhohofisha kabisa timu ya mbeya city, Na mpira ulikuwa umeisha tu mara baada ya amisi tambwe kuipatia yanga gori la tau dakika ya 82 hali ilyofanya kuongoza hadi filimbi ya mwisho.
Bao la Mbeya city liliweza kupatikana dakika ya 68 kupitia Peter Mapunda aliyeonganishiwa mpira mzuri sana kutoka kwa Deus Kiseke.
Ni mfulululizo mgumu sana ambao Mbeya City kupata vipigo hivi na mashabiki watimu mbalimbali hawakuamini kama mambo yanaweza kuwa hivi kwa timu hii. Ukiona mwenzio ananyolewa nawe tia maji, Prison inatakiwa ijiandae kwa hili!