Mourinho; Mimi ni bora na ni wa kipekee
Kocha mwenye maneno mengi na pia mwenye mafanikio mazuri katika ulimwengu wa Soka barani Ulaya maarafu kama Mourinho ajigamba mbele ya vyombo vya habari juu ya uwezo wake.
Kujiamini huko kwa kocha kumekuja tu mara baada ya kuwa na gap kubwa kati ya timu yake ya Chelsea na mpinzani wake wa mwaka huu Manchester city, kwa kuweza kutangulia point 5 mbele na viporo 2,
Mourinho katika mahojiano yake na waandishi wa habari aliweza kujisifia uwezo wake kwa kulinganisha na makocha wengine barani Ulaya, Kwa maelezo yake Mourinho alisema hivi;
``Watu wengi wananionea huruma mimi kuliko wanavyojionea wao, hawajui furaha yangu ni nini? furaha yangu zaidi ni vile navyojilinganisha mimi zidi ya makocha wengine, nikijarabu kuangalia wao naona ni mafanikio madogo sana kuliko mimi,
``Angalia katika Mashindano ya Uingereza, nani ni bingwa wa Ulaya, mimi au Van Gal?
angalia katika kutwaa vikombe vya ligi kuu kati ya mimi AU Wenger?
``Haya ni mambo yanayonifanya nijione kuwa mimi ni bora na wa kipekee na sijali upuuzi ambao upo kwenye vyombo vya habari juu yangu.
Akuishia hapo tu, pia aliweza kufanya mlinganisho juu ya utwaaji wa makobe ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kujilinganisha na Carlo Ancelotti na Guardiola na Van Gal.
