FALCAO AHAIDI MASHABIKI WA CHELSEA HAYA KATIKA MECHI ZIJAZO
Mshambuliaji wa mkopo wa timu ya Chelsea Radmel Falcao ahaidi kufanya vizuri katika mechi za Chelsea zijazo licha ya kutofanya vizuri katika mchezo uliopita zidi ya Southapmton.
Falcao ambaye alikuwa mchezaji wa Atletico Madrid yupo katika kipindi kigumu mara baada ya kiwango chake kushuka alipoumia katika klabu yake ya Monaco.
Licha ya mchezaji huyo kutopata nafasi za kutosha kuanza katika klabu hiyo toka aliponunuliwa hapo kwa mkopo ana matumaini kabisa ya kurudi kiwango katika mechi zijazo.
