CARLO ANCELLOTI AFUNGUKA KUHUSU KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED
Kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na ile ya Real Madrid Ancelotti afunguka kuhusu nia yake ya kupenda kuifundisha Manchester United katika kipindi hiki.
Alipohojiwa na mmoja wa wahandishi wa habari za michezo alisema ya kuwa alikuwa na mapenzi ya dhati ya kuifundisha Manchester United toka muda mrefu na hivyo itakuwa ni vizuri kwake endapo atachaguliwa kwenda kuifundisha timu hiyo katika kipindi hiki kwa kuwa bado anapenda kufundisha soka nchini Uingereza.


