MOURINHO AIBUKA NA HILI KATIKA ULIMWENGU WA MICHEZO SIKU CHACHE BAADA YA KUFUKUZWA CHELSEA
Kumekuwa na tetesi nyingi katika magazeti mengi duniani ya michezo kuhusu Mourinho ambapo mengi yalielezea ya kuwa huenda kocha huyo atapumzika kidogo katika soka ili kuweza kujipanga upya katika fani yake kitu ambacho sicho. Leo hii Mourinho amedhihirisha ya kuwa anapenda kuendelea na Soka na hivyo hatachukua mapumziko huku akionekana kupenda kuendelea kufundisha Uingereza na sio nje ya hapo kama jinsi ilivyoelezwa na baadhi ya magazeti.
