VAN GAL APAZA SAUTI KWA MASHABIKI WA MAN U KUHUSIANA NA MFULULIZO MBAYA WA MATOKEO
Kocha mkuu wa Manchester United aeleza ya moyoni kuhusiana na mfululizo mbaya wa matokeo ya klabu ya Manchester United katika kipindi hiki.
Akiongea na waandishi wa habari alisema ya kuwa mfululizo huo wa matokeo mabovu katika mechi 6 zilizopita umewafanya mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na imani na Kocha huyo na hivyo kuwafanya wengi kumzungumzia yeye juu ya hali hiyo ila yeye anachokijali ni sapoti ya wachezaji tu na hivyo haimkatishi tamaa kusonga mbele kama jinsi inavyotabiliwa.
