JOSE MOURINHO AFUNGUKA KUHUSU SABABU ITAKAYOMFANYA AONDOKE CHELSEA
Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho afunguka mazito kuhusu kitu kitachomfanya aondoke Chelsea katika kipindi hiki.
Akiongea na waandishi wa habari jana Uingereza kocha huyo alisema ya kuwa ikiwa wachezaji wake watamchukia na kutomtaka basi hataona sababu ya kuendelea kuwepo katika klabu hiyo na hivyo hatajiuzuru ukocha.
Kabla ya maneno hayo Mourinho pia aliuonya uongoza wa timu hiyo ya kuwa utafanya makosa makubwa sana ikiwa kama itafukuza kazi yeye kwa maana anaamini ya kuwa hakuna kocha bora katika klabu hiyo kama yeye na haitakuja tena kumpata.
Maneno hayo yamesemwa mara baada ya timu ya chelsea kuwa katika headline za magazet mengi na vituo vingi vya duniani mara baada ya kuwa katika kiwango kibaya sana huku wakifungwa kila kukicha.
Japokuwa Chelsea ipo katika wakati mgumu kama huu mashabiki wake wengi wamekuwa wakisusia mechi katika mechi zilizopita kutokana na matokeo mabovu ila hawajaonyesha dalili yeyote ya kuchoshwa na kocha huyo.
